Baada ya Beyonce Kuachia Album Yake Mpya Kimyakimya, Aamua Kufunguka ni Kwa nini Ameamua Kuachia Video Pamoja na Audio 31 Kwa Mpigo

Katika Siku ya Jana ambayo ilikuwa ni December 13, mke wa Jay Z na mama wa Blue Ivy, Beyonce Knowles aliwa-surprise mashabiki wa muziki duniani kwa kuachia album yake ya 5 ‘Beyonce’ bila taarifa wala kufanya promo ya aina yoyote. Hilo peke yake halikutosha, kubwa lingine ameachia album hiyo yenye nyimbo 14 (audio) na (video) zake 17 kwa wakati mmoja.


Beyonce amezungumzia sababu za kutoa album yake mpya kwa mtindo huo na kudai kuwa watu wamekuwa hawapati muziki kama wanavyostahili kuupata,


“Now, people only listen to a few seconds of a song on their IPODS, they don’t really invest in a whole album. It’s all about the single and the hype. There’s so much that gets between the music, and the artists and the fans. I felt like, I don’t want anybody to give the message when my record is coming out. I just want this to come out when it is ready, and from me to my fans.” Alisema Bey.

Queen Bey ameendelea kusema kuwa alipowaambia timu yake kuwa anataka kushoot video kwa kila wimbo wa albam hiyo ili aje kuzitoa kwa pamoja, kila mmoja alidhani amechanganyikia, “but we’re actually doing it, it’s happening!’ Alisema.

“I wanted everyone to see the whole picture, and to see how personal everything was to me. I will make my best art and just put it out. And that’s why it’s out today!”.

Fahamu Vitu Vitano Muhimu kuhusu albam mpya ya Queen Bey iitwayo ‘Beyonce’

1.Albam hiyo imechukua mwaka mmoja na nusu kuandaliwa.

2.Video 17 za album hiyo zimeshutiwa wakati za ziara zake za ‘Mrs Carter World Tour’ katika sehemu mbalimbali alizotembelea, zikiwemo maeneo ya beach nchini Brazil, Paris, nk.

3.Album ilianza kuandaliwa summer 2012, baada ya waandishi na maproducer kukusanyika chini ya paa moja huko The Hamptons na kuishi pamoja, kufanya kazi pamoja, na kuingia katika dunia ya Bey ili kupata mawazo yake.

4.Kuna orodha ndefu ya waandishi, producers na video directors waliohusika katika project hiyo wakiwemo mume wake Jay Z, producer mkongwe Timbaland, Justin Timberlake, Pharrell Williams, Drake, The Dream, Sia, Miguel, Frank Ocean, Hit Boy, Ammo, Boots, Detail, Hype Williams, Terry Richardson, Melina Matsoukas, Jonas Akerlund, Noah “40″ Shebib, na wengine.

5. Album hiyo kwa sasa inapatikana exclusively katika Itunes kwa wiki moja, na itaingia katika soko la kawaida December 21.


SOURCE: NECOLE BITCHIE

Previous Post Next Post