Picha: Wengi Kumzika Nelson Mandela, Watu Walia,Waumia Wakigombania Kumuaga Kwa Mar Ya Mwisho.

Wananchi wa South Afrika Pamoja na Wageni Waliofika nchini Hapo kwa nia ya dhati kabisa kutoa pole na kuaga mwili wa Hayati Nelson Mandela jana nsio ilikuw siku ao ya mwisho kuuaga mwili huo, Barabara zilifungamana kwa umati mkubwa wa watu ambao walitaka kumuaga Baba wa Taifa Lao.

Hizi ni Picha Chache zinazoonyesha jinsi gani hali ilivyokuwa South Africa 


Polisi wakijaribu kuwazuia watu wasiendelee kuingia

Kutokana na umati mkubwa uliojitokeza, polisi walijaribu kuzuia watu wasiendelee kuingia kwa kufunga mageti, lakini hata hivyo watu hao walilisukuma na kutaka kuingia kwa nguvu ili na wao wakatoe heshima zao za mwisho.

LD-10





Huko kijijini Qunu ambako mwili wa Mandela unatarajiwa kupelekwa leo tayari kwa mazishi yatakayofayika kesho Jumapili, maandalizi yako katika hatua za mwisho.

                                         Sanamu ya Mandela ikimaliziwa


Siku ya Jumatatu (December 16) baada ya mazishi, Rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma anatarajiwa kuzindua sanamu ya Nelson Mandela, ambayo imeonekana ikimaliziwa kuwekwa katika ofisi za Serikali ‘Union Buiildings’ jijini Pretoria jana.



Kijijini Kwao Nelson Mandela 'Qunu', maandalizi ya mwisho yakifanywa tayari kupokea mwili kwa mazishi kesho
Previous Post Next Post