YULE ALIYEUA MMOJA, NA KUJERUHI 3 AKIWEMO MCHUMBA WAKE KWA RISASI,NAYE KUJIUA UBE ALIPANGA MUDA MREFU TOKA SEPT KUTITIA FACEBOOK

Mfanyabiashara wa magari jijini Mwanza, Gabriel Munisi (35), aliyejiua juzi baada ya kumuua mtu mmoja na kujeruhi wengine watatu jijini Dar es Salaam katika tukio linalohusishwa na wivu wa mapenzi, alikuwa amepanga kufanya hivyo tangu September mwaka huu.





September 18 mwaka huu kupitia ukurasa wake wa Facebook, Gabriel ambaye wengi walikuwa wakimuita Gabu, aliandika:

Najua mtasema sana ila hakuna anaejua ukweli zaidi yangu mm muhusika na najua wazi mengi mtawaza na hamtopata majibu yake…. (Remember all things are possible).



Katika tukio la jana, Munisi, aliwapiga risasi watu watatu akiwemo mchumba wake, Christina Alfred katika Mtaa wa Bungoni Wilaya ya Ilala, Dar es Salaam.

Baada ya kumpiga risasi mchumba wake huyo na kudhania kwamba amemuua, inadaiwa kwamba Munisi aliendelea kuwamiminia risasi watu wengine na kumuua mdogo wake Christina, Alpha (22).

Katika tukio hilo, Christina na mtu anayedaiwa kuwa mchumba wake mpya, Francis Shumila wamelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kujeruhiwa. Mama yake Christina, Helen Alfred amelazwa katika Hospitali ya Amana baada ya kujeruhiwa pia.


Gabriel baada ya kujipiga risasi na kufa hapo hapo

Gazeti la Mwananchi limeandika kuwa mashuhuda waliokuwapo katika tukio hilo walisema mauaji hayo yalitokea saa 1.15 asubuhi baada ya Munisi kufika Ilala Bungoni na kwenda katika Klabu ya Wazee iliyo jirani na eneo yalipotokea mauaji na kunywa supu kabla ya kusogea karibu na lango la nyumba anakoishi mchumba wake.

Mmoja wa majirani, Noel Gerald alisema alimuona Munisi akiwa amesimama karibu na lango la nyumbani kwa kina Christina.

Alisema baadaye waliona gari aina ya Toyota Hilux, Surf, likitoka katika lango la nyumba hiyo na mara walimuona Munisi akimwamuru dereva ashushe kioo lakini alikataa na kudai kwamba ndipo alipoamua kuwapiga risasi waliokuwamo kwenye gari hilo.

Alidai kuwa Munisi alipiga risasi nane mfululizo huku akiwa analizunguka gari hilo na kwamba alimpiga dereva ambaye baadaye alifahamika kuwa ni Shimula. Imeelezwa kuwa majeruhi huyo ni raia wa Kenya na ni rubani wa ndege.
“Katika gari lile walikuwemo watu watatu ambao ni Christina, Helen na Shimula, ambaye alikuwa ndio dereva huku marehemu Alpha akiwa getini na Munisi alimpiga risasi ya kifua,” alidai Gerald.

Shuhuda huyo alidai kwamba Munisi aliendelea na mashambulizi yake kwani magazini ya kwanza ilipomaliza risasi katika bastola yake, aliongeza nyingine na kumfuata mama yake Christina ambaye pia alikuwa ndani ya gari hilo, na kumpiga risasi mkononi.

Alidai kwamba alipona baada kutoka na kukimbilia uvunguni mwa gari.

Alisema baada ya kufanya mauaji hayo, Munisi aliamua kujipiga risasi ya kifuani na kufariki papo hapo akiwa amekaa karibu na lango hilo.

Ilidaiwa kwamba Shimula na Christina walikuwa wanaelekea Uwanja wa Ndege wa Mwalimu Julius Nyerere kuelekea Visiwa vya Cyprus.

Rafiki wa Munisi aliyejitambulisha kwa jina la Samwel Alex alisema Christian alikuwa mchumba wa Munisi na walikuwa wamepanga kuoana.

Alisema Munisi baada ya kuwa na wasiwasi na mchumba wake ndipo alipoamua kumpigia simu mama mzazi wa Christina na kumwambia kuwa amesikia mwanaye yupo hapo Dar es Salaam lakini alikataa na kumweleza kuwa amesafiri kwenda Moshi.

“Ninawafahamu kwa muda mrefu, Christina alikuwa anafanya kazi Barclays Bank na Munisi ni mchumba wake wa muda mrefu kwani alikuwa anajulikana hata kwa ndugu zake wote,” alisema Alex.

Source: Mwananchi, Facebook.
Previous Post Next Post

Popular Items