POPPIN VIDEO: VIDEO MPYA NA ILIYOTAZAMWA NA IDADI KUBWA YA WATU KWA SIKU 4

Mafanikio ya kazi mpya ya member wa zamani wa Wakilisha Sarah Kaisi aka Shaa yameanza kuonekana mapema kutokana na mapokeo mazuri aliyoyapata katika kipindi kifupi toka wimbo wake mpya ‘Sugua Gaga’ utoke wiki iliyopita.



Kwa mujibu wa Shaa mwenyewe, video ya ‘Sugua Gaga’ imevunja rekodi iliyowekwa na video zake zote zilizopita ikiwemo ‘LavaLava’, kwa kutazamwa mara 20,000 ndani ya siku tatu toka iwekwe youtube September 31.
“shaa_tz Oyooooooo its official.. #SuguaGaga imevunja rekodi ya #LavaLava na single zangu zote… #20,000hits on Youtube ndani ya siku 4 tu! #shidaaaaa Nawashukuru wote.. #TeamShaa”Shaa alishare mafanikio hayo Instagram juzi



.

Mpaka sasa video hiyo ambayo imefanyika Magomeni, Dar es salaam imefikisha hits 
31,871 views ikiwa ni siku 5 toka imewekwa youtube.

Sugua Gaga ni kazi ya kwanza kutoka kwa Shaa chini ya mkataba aliosaini na ‘Mkubwa na Wanae’ ya Said Fella kwa lengo la kumsimamia kwa miezi sita huku wakifanya nyimbo zitakazowalenga watu wa hali ya kawaida kabisa ambao nyimbo zake za mwanzo zimekuwa zikiwabagua.

Previous Post Next Post