Picha: Azam TV kuingia hewani mwezi ujao

Kampuni ya Azam TV inatarajia kuanza rasmi matangazo yake mwezi ujao. Azam TV itakuwa ikitoa huduma ya matangazo ya TV ya dijitali kwa kutumia satellite ikiwa na king’amuzi chake ambacho tofauti na vingine itakuwa na malipo ya aina moja tu.

Cameraman wa Azam TV akiwa kazini

Ikiwa imeanzishwa mwaka huu pekee, Azam TV imepanga kupanuka zaidi na kuzifikia nchini nyingi za Afrika. Imedai lengo lake ni kuwa na vipindi vya aina mbalimbali kutoka channel za ndani na nje vinavyozifaa familia na watu wa kila rika.


Pamoja na kuwa na channel zingine zipatazo 50, Azam TV itakuwa na TV zake tatu ambazo ni Azam One itakayokuwa ikionesha vipindi vya Kiafrika hasa vya Kiswahili, Azam Two itakayokuwa ikionesha channel za kimataifa ambapo vipindi vingine vitatafsiriwa kwa Kiswahili.


Pia kutakuwepo na channel ya Sinema Zetu ambayo itaonesha filamu za Tanzania saa 24.

Kampuni hiyo imejenga studio mbili kubwa zilizopo Tabata ambapo hadi January 2014 zitaanza kurekodi vipindi vya ndani na vya maongezi (talk shows).

Wafanyakazi wa Azam TV wakiwa pamoja na waandishi wa habari waliotembelea studio zao
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA