Jana tuliitisha kura za maoni Facebook na Twitter kutaka kufahamu kutoka kwa wasomaji wetu kuwa ni mtangazaji gani wa radio nchini mwenye ushawishi mkubwa na anayesikilizwa zaidi kuliko wengine.
Tanzania imeongea, na tunamtambulisha mtangazaji anayependwa zaidi, mwenye ushawishi kuliko wengine na ambaye kipindi chake husikilizwa zaidi, kuwa ni Millard Ayo aka ‘Mtu wa Nguvu’, wa Clouds FM.
Tanzania imeongea, na tunamtambulisha mtangazaji anayependwa zaidi, mwenye ushawishi kuliko wengine na ambaye kipindi chake husikilizwa zaidi, kuwa ni Millard Ayo aka ‘Mtu wa Nguvu’, wa Clouds FM.
Japo si kituo chake cha kwanza kuanza kazi, jina la Millard lilianza kufahamika nchini kupitia kipindi cha Milazo 101 cha Radio One. Sauti yake yenye mamlaka na ubunifu hewani, ulikifanya kipindi hicho kuwa maarufu kuliko vingine vya burudani katika radio hiyo inayomilikiwa na kampuni ya IPP.
Kuondoka kwake Radio One kulikuwa ni pigo kubwa lakini lenye neema kwa Clouds FM. Alihamia Clouds FM na kuanzisha kipindi kipya kiitwacho Amplifanya ambacho kilichukua nafasi ya kipindi cha nyimbo za kiafrika, Bambataa. Haikuchukua muda kipindi cha Amplifanya kikawa miongoni mwa vipindi bora kabisa Clouds FM. Kipindi hicho pia ni miongoni mwa vipindi vinavyoiingizia fedha nyingi redio hiyo na kumfanya Millard kuwa miongoni mwa watangazaji wa kituo hicho wanaolipwa mshahara mkubwa zaidi.
Leo hii Millard ni miongoni mwa watangazaji bora Tanzania na wanaosikilizwa zaidi. Si maarufu tu redioni bali pia ndiye mtangazaji wa Tanzania mwenye mashabiki wengi zaidi kwenye mitandao ya kijamii. Ana zaidi ya followers 67,000 kwenye Twitter huku Facebook akiwa na likes zaidi ya 145,530.
Umaarufu wake kwenye mitandao ya kijamii umemfanya ageuke brand na kuyavutia makampuni makubwa kama CRDB Bank, Fast Jet na mengine kudhamini kile anachotweet. Tweets zake tu zinamuingizia fedha huku akimiliki pia website yake binafsi yenye wasomaji lukuki na yenye matangazo mengi.
Kwa mshahara anaoupata, kazi ya uripota wa DSTV, ubalozi wa Fastjet, website yake, deal za voice-overs na mambo mengine, Millard anaingiza takriban ama zaidi ya shilingi milioni 10 kila mwezi.
Millard ni zaidi ya mtangazaji, bali ni mwandishi mwenye ‘pua ya habari’ (nose for news) huku akiongoza kwa kuja na angle za kipekee za habari zenye mvuto kwa watu (human interest stories) zinazokifanya kipindi chake cha Amplifaya kuteka matangazo ya jioni siku za wiki.
Pamoja na kupata mafanikio hayo, Millard ameendelea kuwa mchapakazi, simple, mtu anayejituma kutafuta habari hata sehemu za mbali kabisa, mcheshi na mtu wa watu.
Hakuna shaka kuwa, Millard ana mustakabali wa nguvu kwenye fani hiyo. Ni mfano wa kuigwa kwa watangazaji wengine na hazina kubwa kwa wazazi wake, Clouds Media Group na hata taifa kwa ujumla.
-Bongo5