Lulu akanusha kuchumbiwa, asema kuolewa kupo tu, lakini bado sana

Mwanadada mwenye jina na  muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha fununu zilizoandikwa kwenye gazeti la udaku liitwalo ‘Filamu’ kwamba amechumbiwa na muda mchache ataolewa.
Akizunguza Leo kwennye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muigizaji huyo wa Foolish Age, alisema hajachumbiwa na mtu yeyote ila ni magazeti ya udaku tu ndio yamekuwa yakiandika kile yanachojisikia.

“Mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote aliyenichumbia na kama itatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua, na ni mimi mwenyewe ndiye nitakaesema,” alisema mrembo huyo.

“Lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari kutoka kwenye chanzo gani, by the way kwaajili kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu anayejisikia kuandika anaandika ,anaamka anaandika, anaamka anandika. Kwahiyo leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, kwahiyo inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo, kwamba ‘leo Lulu tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe’, I don’t know.

“Kuchumbiwa, kuolewa,kuwa mke ni vitu ambavyo tumeumbiwa binadamu, vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa.”

Previous Post Next Post

Popular Items