Kitabu cha Sir Alex Ferguson ‘My Autobiography’ chavunja rekodi kwa kununuliwa kama ‘njugu’

Kitabu cha Sir Alex Ferguson, kimevunja rekodi kwa kuwa kitabu kisicho na mambo ya kutunga (non-fiction) kinachouzika kwa kasi zaidi.


Kitabu chake kilichokuwa kikisubiriwa kwa hamu kiitwacho ‘My Autobiography’, kimeuza kopi 115,547 katika wiki moja.

Kitabu cha Fergie ambacho kinauzwa kwa paundi £25 – kimeuza zaidi kwa wiki moja tangu miaka 15 iliyopita, kwa mujibu wa jarida The Bookseller. Rekodi ya awali ilishikiliwa na kitabu cha Delia Smith, How To Cook: Book Two kilichouza kopi 112,000 katika wiki ya kwanza, miaka 14 iliyopita.


Kitabu cha Sir Alex kimezidi vitabu vingine vya watu maarufu wa Uingereza kama kile cha Tony Blair, A Journey kilichouza kopi 92,000 miaka mitatu iliyopita na cha David Beckham, My Side, kilichouza kopi 86,000 katika wiki ya kwanza miaka 10 iliyopita.


Previous Post Next Post