HEMEDY PHD KUJA NA KITU KINGINE KIPYA, MAKIN ZAIDI...

Rest Of My Life’ ni moja ya ngoma ambayo inafanya vizuri sana kwenye chati mbalimbali za muziki hapa Tanzania na nje pia, ambayo imeachiwa siku za karibuni tu na kufanyiwa video iliyoifanya ngoma hiyo kung’aa zaidi …


Hemed PHD, hajaishia hapo, sababu kwa sasa anatarajia kuachia ngoma nyingine kali zaidi ambayo itakwenda kwa jina la “One And Only” ambayo atamshirikisha msanii mwingine mzuri ‘Bellacombo’.


Pia msanii huyu mahiri aliongeza kwa kusema kuwa baada ya kuachia ‘One And Only’, mashabiki wake wategemee kuona video kali zaidi ya wimbo huo kutokana na kwamba amejipanga kikamilifu kuanzia Budget nzuri hadi production nzuri ya video kutoka kwa ‘Kwetu Studios’ na anaamini kuwa ukiwa na team nzuri iliyojipanga haiitaji kufanyia video nje ya nchi, cha msingi ni kijituma na kuwa na maandalizi ya budget nzuri ndiyo yatafanya kazi isimame.

Mashabiki wa Hemed PHD wategemee ujio wa video ya wimbo huo mpya atakao uachia mwezi huu tarehe 22, kuwa video yake itatoka rasmi tarehe za mwanzo wa December na itazinduliwa katika show kubwa ambayo atifanya kwa ajili ya kuenzi safari yake ya muziki tangu alipoanza mpaka alipofikia sasa.
Previous Post Next Post