QUICK RACKA KUACHIA HIT NYINGINE KALI SANA ALIYOMSHIRIKISHA AY NA SHAA COMINFG SOON

“My Baby”…Ustadi makini uliotumika kwenye utengenezaji wa mdundo huu ulioambatana na mashairi mazuri, ndiyo sababu kubwa inayomfanya QUICK ROCKA a.k.a SWITCHER kuendelea kufanya vizuri katika music industry …

That’s right !! Yule mkali ambaye alisimamia vyema Chorus ya mdundo uliobamba na unaoendelea kuwa na kick kwenye ngoma kali za Town, unaojulikana kama Ball Player as well as ‘Jana Na Leo’, anakuja tena na nyingine hivi karibuni…


Quick alisema yupo mbioni kuangusha ngoma yake nyingine itayokwenda kwa jina la MAASAI ambayo atakuwa alongside Mzee wa Commericial, AY pamoja na mwanadada Shaa – mkali wa Sugua Gaga ,single ambayo imepokelewa vyema na wapenzi wa burudani wa muziki nchini na kwingineko..

“Tarehe 28 mwezi huu wa Novemba nategemea kutoa MAASAI niliyomshirikisha AY na Shaa”, alisema Quick. Pia akaongeza kwa kusema, production ya ngoma MAASAI imefanywa na DANNY & Master J.

Bila shaka, hii itakuwa nyingine ya aina yake kwani Bongo Flava inaendelea kufanya vizuri kutokana na umakini pamoja na kujituma kwa wasanii katika kuhakikisha kazi zao zinakuwa za uhakika na zitazokubalika na jamii…

Previous Post Next Post