CRIS BROWN "NAITAJI SANA BANGI KULIKO LAPTOP NA SIMU YANGU"

Mkali wa Rn'B na Pop Chris Brown ametoswa ruhusa ya kuvuta bangi ndani ya rehab. TMZ imeripoti kuwa Chris alikuwa hiari kukabidhi simu yake na laptop wakati akiingia kwenye rehab lakini akanyimwa ruhusa ya kuingia na bangi aliyodai anaiihitaji sana.


Chris anadaiwa kuwaambia madaktari aliandikiwa na daktari kutumia bangi kwakuwa inamsaidia kumweka sawa kiakili. Alisema bangi humsaidia kumtuliza lakini bado wafanyakazi walimtosa.

Anatakiwa kukaa kwa siku 90 ndani ya rehab kusaidia kupunguza tatizo lake la kuwa na hasira ambapo awali kabla ya awamu hii alikuwa amekaa siku 16 lakini alifukuzwa baada ya kufanya fujo na kudaiwa kuiponda jiwe gari ya mama yake.
Previous Post Next Post

Popular Items

WAKUU WA USALAMA KUHOJIWA KENYA