BODI YA BARAZA LA SANAA-TANZANIA WATANGAZA NEEMA KWA WASANII WA BONGOMOVIE

Wajumbe wapya wa Bodi ya Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA), wametaka kupewa miezi sita ili wasanii waanze kufaidi matunda yao


   Alex Msama

Akizungumza na gazeti la Mwananchi juzi, Alex Msama kwa niaba ya wajumbe wenzake wa bodi hiyo iliyozinduliwa hivi karibuni, alisema BASATA ina changamoto nyingi ikiwemo kukosa vyanzo vya kutosha vya mapato hivyo changamoto waliyonayo ni kuhakikisha inajiendesha yenyewe.

“Tutaboresha kazi za wasanii kwa kuziinua na kuzilinda kwa nguvu zote, tutasimamia studio zitoe kazi bora za wasanii sio bora kazi, tunataka ifike mwisho wasanii kwenda kurekodi Afrika Kusini, China na kwingineko na kazi zetu zivuke mipaka,” alisema.

“Ndani ya miezi sita, matunda yetu yataanza kuonekana, kikubwa tunaomba ushirikiano kwa wasanii na wadau wote wa Sanaa,” alisema Msama.
Previous Post Next Post

Popular Items