Mechi ya watani wa jadi Simba na Yanga Jumapili hii imemalizika kwa sare ya mabao 3-3 kwenye uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam. Hiyo ilikuwa ni mechi iliyokuwa ushindani mkubwa ambapo Yanga katika kipindi kwa kwanza ilifanikiwa kuifunga Simba mabao matatu hali iliyowafanya mashabiki wa Simba wanyong’onyee kwa kuamini kuwa wamepoteza mechi hiyo.
Kipa wa Simba aliumia shingo baada ya kubabatizana na mchezaji wa Yanga katika harakati za kulinda lango
Mashabiki wa Simba wakiongozwa na muigizaji wa filamu nchini Jacob Stephen aka JB wakiwa na nyuso za huzuni na zilizokata tamaa baada baada ya Simba kufungwa mabao 3 katika kipindi cha kwanza
Mchezaji wa Yanga, Jerry Tegete akiwalaumu wachezaji wa ndani baada ya Simba kusawazisha goli la 2 katika kipindi cha pili
Mrisho Khalfan Ngassa ndiye aliyekuwa wa kwanza kuwanyanyua mashabiki wa Jangwani kwa kufunga bao la kwanza katika dakika ya 15. Dakika ya 36, Hamisi Kiiza aliiandikia Yanga bao la pili katika mpira wa kurushwa na Mbuyu Twite.
Kipa wa Simba aliumia shingo baada ya kubabatizana na mchezaji wa Yanga katika harakati za kulinda lango
Katika dalili ya wazi kuwa bahati ilikuwa kwa Hamisi Kiiza, mchezaji huyo aliitikisa tena nyavu ya Wekendu wa Msimbazi na kuifanya idadi ya magoli kuwa 3 bila, hali iliyoendelea hadi timu hizo zilipoenda mapumziko. Pamoja na Yanga kupata magoli matatu, walikitawala kipindi chote cha kwanza hali iliyowafanya Simba waonekane kama ‘Waanagenzi’ tu.
Mashabiki wa Simba wakiongozwa na muigizaji wa filamu nchini Jacob Stephen aka JB wakiwa na nyuso za huzuni na zilizokata tamaa baada baada ya Simba kufungwa mabao 3 katika kipindi cha kwanza
Kama vile waliamshwa usingizi, wachezaji wa Simba waliingia uwanjani kwenye kipindi cha pili wakiwa na nguvu za ajabu na kuanza mashambulizi yaliyoivunja ngome ya Yanga. Haikuchukua muda mrefu, nguvu mpya za Simba zikaanza kuzaa matunda.
Katika dakika ya 54 tu, Betram Mombeki alifunga goli la kwanza la Simba. Wakati Yanga ikiwa inaanza kulionja joto la ghafla kutoka kwa Simba na kujipanga kulinda ngome yao isivunjwe tena, katika dakika ya 58 Joseph Owino aliandika bao la 2 lililozalishwa na krosi maridadi kutoka kwa Ramadhani Singano aka ‘Messi’.
Goli la pili liliwapa nguvu zaidi Simba waliondelea kuwashambuliwa Yanga kwa kasi. Katika hatua hiyo wachezaji wa Yanga walianza kujichanganya na kuwadhoofisha zaidi hadi kumpa mwanya beki Kaze Gilbert kusawazisha goli la tatu na kuvifanya vibao vya magoli uwanjani humo kusomekaYanga 3 – Simba 3.
Tazama picha zaidi za mambo yalivyokuwa kwenye mechi hiyo.
kumalizika-kwa-sare-ya-3-3..jpg”>
Shabiki wa Yanga aitwaye Athuman Kombo akilia kwa uchungu baada ya mchezo wa Yanga na Simba kumalizika kwa sare ya 3-3
Shabiki wa Yanga aitwaye Athuman Kombo akilia kwa uchungu baada ya mchezo wa Yanga na Simba kumalizika kwa sare ya 3-3
Image Credit: by Bongo5
Tags:
Sports