PICHA: SUMA MNAZALETI KUFANYA WIMBO NA BUSY SIGNAL, NA ADAI KUTUMIA ZAIDI YA MILL 30 KUSHOOT VIDEO YAKE MPYA

Suma Mnazaleti amesema ametumia zaidi ya shilingi milioni 30 za Kitanzania kushoot video ya wimbo wake Asante nchini Afrika Kusini.


Suma Mnazaleti akiwa na model kwenye moja ya scene ya video hiyo iliyofanyika jijini Cape Town

“Ni zaidi ya 30, sio milioni 30 peke yake,” Suma alikiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio leo, Jumamosi. Alisema pesa hizo ni za kwake mwenyewe na hakuna aliyemsaidia na kuongeza kuwa uzinduzi wa video yake utafanyika November 1 kwenye jijini Mbeya.


“Video yangu haitazinduliwa Dar es Salaam kama watu wanavyotegemea hiyo ilikuwa nataka niwaoneshe watu utofauti,” alisema.

Katika hatua nyingine, Suma alidai kuwa mwezi December ataenda nchini Jamaica kufanya video ya wimbo wake, Umechelewa na huko atafanya collabo na msanii wa dancehall, Busy Signal.

“Nina collabo na Busy Signal. Naitangaza rasmi kwasababu kila kitu kipo mezani, vitu vyote vishaisha ni safari yangu tu. Watu wasubiri tu collabo ambayo itatoka January na Busy Signal kutoka Jamaica.”


Previous Post Next Post