KUELEKEA KOMBE LA DUNIA LITAKALO FANYIKA BRAZIL 2014, ROONEY NA GERRARD WAIOKOA ENGLAND

Wachezaji wa England wakishangilia ushindi (HM)


MABAO ya Wayne Rooney na Nahodha Steven Gerrard yameihakikishia England nafasi ya kucheza Kombe la Dunia usiku huu baada ya kuifunga Poland 2-0 usiku huu kwenye Uwanja wa Wembley.
Kikosi cha Roy Hodgson jana kimewapa raha Waingereza kwa ushindi huo na sasa ni furaha nchi nzima England.
Mshambuliaji wa Manchester United, Rooney alianza kufunga dakika ya 41 na kiungo wa Liverpool, Gerrard akafunga dakika ya 88.
Kikosi cha England kilikuwa: Hart, Smalling, Cahill, Jagielka, Baines, Gerrard, Carrick/Lampard dk71, Townsend/Milner dk86, Rooney, Welbeck na Sturridge/Wilshere dk82.
Poland: Szczesny, Wojtkowiak, Jedrzejczyk, Glik, Celeban, Blaszczykowski, Mierzejewski/Zielinski dk75, Krychowiak, Sobota/Pezsko dk65, M Lewandowski/Klich dk46 na R Lewandowski. 

Source: Sportmail 
Previous Post Next Post