In My Shoes : Ni Reality Show Mpya ya Wema Sepetu Itakayoanza kuonekana Jumatano Hii ndani ya EATV



Hapo kabla star wa bongo anayeongoza kwa ‘ndrama’, Wema Sepetu alikuwa akionekana zaidi katika magazeti, na mara kadhaa kupitia matukio mbalimbali katika TV, lakini kuanzia Jumatano hii ataanza kuonekana kupitia kipindi chake kipya cha runinga ‘In My Shoes’.







Kama umeshawahi kukutana na Wema katika event yoyote na ukawa unajiuliza maswali kwa kuona jinsi alivyozungukwa na crew ya watu wanaomfuata na Camera zikiwa on kila anapoelekea, sasa utaanza kupata majibu ya maswali hayo kuanzia wiki hii.

Kipindi cha kwanza cha ‘In My Shoes’ cha CEO wa Endless Firm kitaanza kuonekana Jumatano hii ( October 16) kuanzia saa 3 na nusu usiku kupitia East Africa Television (EATV).

Mastaa wengine ambao tayari walikuwa wameiona fursa na kuanzisha reality show zao ni pamoja na Lady Jay Dee ambaye anakipindi kinaitwa ‘Diary’ ambacho huoneshwa kupitia EATV, na mwingine ni Irene Uwoya ambaye kipindi chake cha ‘Paradise’ huoneshwa kupitia Clouds TV.
Previous Post Next Post

Popular Items