Audio: Diamond kumfuata Davido Nigeria kufanya video ya ‘My Number One-Remix’

Story zilizosambaa kwenye mtandao toka juzi ni kuhusu ujio wa remix ya ‘My Number One’ ya Diamond Platnumz aliyomshirikisha star kutoka Nigeria Davido, lakini habari mpya kutoka kinywani mwa Nasib Abdul mwenyewe ni kwamba anatarajia kwenda Nigeria ‘soon’ kufanya video ya wimbo huo baada ya kushindikana kufanyika jana.



Diamond kupitia Instagram juzi aliandika kuwa remix ya ‘My Number One’ ingefanyiwa video jana Jumapili (Oct 27), lakini zoezi hilo lilishindikana kutokana na matatizo yaliyojitokeza katika tamasha la Fiesta Jumapili alfajiri hivyo yeye na Davido kutakiwa kuperform jana jioni.

“Video tulitakiwa tuifanye jana unfortunately kwasababu ya matatizo kidogo yaliyotokea hatukuweza kufanya kwasababu jana tulikuwa tuna performance nyingine, na ndo maana ikabidi tuperform jana pale lakini video tunafanya Nigeria soon nafikiri next week kama sikosei, actually as soon as possible sababu haina muda wa kukaa kusubiria timming.” Diamond amefunguka kupitia Showtime ya Radio Free Africa ya Mwanza leo.
Alipoulizwa na mtangazaji wa kipindi hicho Bizzo kwanini hakuitumia nafasi aliyoipata ya kufanya kazi mpya kabisa na Davido na badala yake kuamua kufanya remix ya Number One, Platnumz amesema kuwa wamefanya vitu vingi siku hiyo ambavyo hayuko tayari kuvisema kwasasa.

“Kwakweli namshukuru mwenyezi Mungu nilifanya vitu vitu vingi kidogo japokuwa vingine siwezi kuvisema kwa sasahivi….wakati wake ukifika nitavizungumzia, kwasababu nikivizungumzia vinaweza hata vikaharibu attention ya hii remix niliyofanya na Davido”. Alisema Diamond.



Diamond na Davido wakiperform ‘My Number One-Remix’ jana Leaders katika tamasha la Fiesta

Akiongezea sababu za kuamua kufanya remix ya Number One, Diamond amesema kwa kufanya hivyo wimbo huo ambao kwa sasa ni hit utapiga hatua zaidi badala ya kuishia Afrika Mashariki, sasa utaweza kupiga hatua zaidi katika nchi zingine za Afrika na baada ya hapo kuna kitu kikubwa kinakuja.

“Then after that naachia mashine nyingine, na hiyo mshine sasa unajua nafanya na nani? Dah itakuwa ni hatari lakini ni kitu kizuri pia”. Kwa maneno hayo kuna uwezekano kama sio Davido basi kuna uwezekano amefanya collabo na msanii mwingine wa kimataifa.

Platnumz ameongeza kuwa kama mipango ingeenda kama ilivyokuwa imepangwa audio ya remix ya My Number One ilitakiwa kuachiwa rasmi wiki ijayo na baada ya siku tatu video ingefata, lakini baada ya ratiba kuvurugika kuna uwezekano wa mabadiliko ya ratiba hiyo.

Msikilize hapa akifunguka zaidi




Previous Post Next Post