Video: Juma Nature: Uhusiano wangu na P-Funk utaendelea kuwa bora zaidi, hatujagombana



Sir Juma Nature alidai kuwa uhusiano wake na producer wa Bongo Records, P-Funk Majani ni mzuri na utaendelea kuwa bora.
Akiojiwa na Mtandao wa  Bongo5 njiani wakati wakielekea Musoma kwenye Serengeti Fiesta, Nature alisema amepunguza kurekodi kwa Majani kwakuwa ana studio yake lakini bado wana uhusiano mzuri.
“Sijatokea muda mrefu sana kufanya recording kwa P-Funk kwasababu sasa hivi mimi nina studio yangu mwenyewe binafsi nikiwa na ndugu zangu Wanaume Halisi. Kiprofessionally P-Funk anatisha,” alisema.
Alesema tayari kuna wimbo wa kushirikisjwa atafanya kwa Majani ambapo Jay Mo na Mchizi Mox nao watakuwemo.
Katika hatua nyingine, Nature alisema yeye ni msanii mkubwa na anaweza kufananishwa na rappers kama KRS One, Mobb Deep au Nas.
“Huwezi kunifananisha mimi na Wiz Khalifa, Wiz Khalifa bwege tu,” alisema.
Previous Post Next Post