PICHA: OMMY DIMPO NA TUPOGO NDANI YA VOA [VOICE OF AMERICA] KUFANYA SHOO KABAMBE LEO JUMAMOSI NDANI YA WASHINGTON DC




Ommy Dimpoz hana ‘phobia’ ya lugha ya Kiingereza na ndio maana hakuukacha mwaliko wa idhaa ya Kiingereza ya Sauti ya Amerika aka VOA kwaajili ya interview jana.



Ommy Dimpoz akiwa kwenye studio za VOA idhaa ya Kiingereza
Hitmaker huyo ambaye yupo nchini Marekani kwa ziara ya wiki tatu ambapo kesho ataperform jijini Washington DC, alizitembelea studio hizo zilizopo kwenye mji huo mkuu wa Marekani kuzungumzia masuala mengi kuhusu muziki wake.


“Nimejifunza vya kutosha kwamba hili ni shirika kubwa sana, wana idhaa 42,” aliongeza.










Kuhusu show yake ya Leo mjini Washington, Ommy amesema: Nimejiandaa vya kutosha, watu wanasubiri kwa hamu hususan Watanzania na Wakenya. Meza za VIP ni sold out tayari, wengine watakata tiketi kwenye show, kiingilio ni dola 30 kawaida.”


Previous Post Next Post

Popular Items