TOKYO KUANDAA MASHINDANO YA OLIMPIKI 2020


tokyo-japan_27ee2.jpg
Tokyo ndiyo mji uliochaguliwa kuandaa mashindano ya olimpiki ya mwaka 2020.Mji huo ulitangazwa kuwa mwenyeji wa mashindano hayo jana mjini Buenos Aires nchini Argentina na kamati ya kimataifa ya olimpiki IOC baada ya kuishinda Istanbul kwa kura 60 dhidi ya 36 katika kura ya siri.Mji wa Madrid ambao pia ulitumai kuandaa mashindano hayo ulibanduliwa mapema katika upigaji kura huo baada ya kutoka sare na Istanbul.(P.T)
Tokyo inayojivunia usalama imeuhakikishia ulimwengu kuwa kuvuja kwa miale ya atomiki kutoka kinu cha nyuklia cha Fukushima kutashughulikiwa kwa wakati ufaao na kuongeza kuwa uvujaji huo haipaswi kuzua wasiwasi kwa maandalizi hayo ya michezo yaOlimpiki. Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe ambaye alihudhuria mkutano huo wa IOC, ameusifu ushindi huo Tokyo na kuahidi kuwa serikali yake italishughulikia tatizo la Fukushima ili kuuhakikishia ulimwengu kuwa Tokyo inastahili nafasi hiyo.
Previous Post Next Post