Kwa mara ya kwanza katika historia ya mji wa Kahama na vitongoji vyake, wakazi wake walipata nafasi ya kuwashuhudia wakali wa muziki zaidi ya 10 katika jukwaa moja katika tamasha la Kilimanjaro Music Tour 2013 lililofanyika katika uwanja wa taiga Kahama na kushuhudiwa na maelfu ya wakazi wa rika zote waliojitokeza na kuujaza uwanja wote. Wakali hao Linex, Profesa Jay, Roma, Ben Pol, Fid. Q, Lady Jaydee, Izzo Bizness, Barnaba na Recho walilishambulia jukwaa kwa masaa sita mfululizo huku wakati mmoja wakipata nafasi ya kumuimbia Ben Pol wimbo wa Birthday kutokana na kuadhimisha siku yake ya kuzaliwa usiku wa kuamkia Jumapili.
Umati wa mashabiki uliojitokeza kuwashuhudia wakali wa muziki mjini Kahama
Linex akilishambulia jukwaa na wimbo wake wa Aifola
Recho na madansa wake katika steji ya Kili Music Tour Kahama
Shabiki mmoja alipata nafasi ya kucheza na Recho
Kutoka backstage: Izzo Bizness, Alice, Fid Q, Kala Jeremiah na Ben Pol
Ben Pol na Alice wakiimba wimbo wao mpya wa Waubani
Ben Pol akiwaimbisha mashabiki kwa hisia
7. Barnaba Boy jukwaani
Linex katika backstage ya Kili Music Tour
Izzo Bishara, Izzo Bizness akiiwakilisha Mbeya mjini Kahama
Izzo Bizness na Barnaba wakishambulia jukwaa kwa pamoja
Baada ya kushuka jukwaani mashabiki hawakutaka kupoteza nafasi ya kupiga nae picha.
Othman Michuzi na wadau wengine wa Kili wakiteta jambo
Hip Hop ikiendelea kuwakilishwa na Kala Jeremiah
Kala Jeremiah akiwauliza mashabiki kama wameilewa Kikwetu kwetu
Jibu la mashabiki lilikuwa ni hili
Roma Mkatoliki akiwarusha mashabiki waliofurika uwanja wa taifa Kahama
Ma-DJ kazini kuhakikisha hakuna kinachoharibika
Linex akiwa na wadau Shaaban Mpondela na Pius toka Frontline Novelli
Lady Jaydee na Profesa Jay wakiimba Joto Hasira
Profesa Jay akiifunga Kili Music Tour Kahama
Mashabiki wakinyoosha mikono juu kuwashukuru wakali wa muziki waliopanda jukwaan
Tags:
live Shows Photos