Jana (September 8) mwanamitindo wa Tanzania Flaviana Matata aishiye Marekani kwa sasa alishiriki katika onesho la mitindo la mbunifu wa Marekani ‘Tracy Reese Spring 2014’.
Flaviana Matata wakati wa onesho hilo
Flavy alivaa nguo iliyobuniwa na mbunifu wa mitindo Tracy Reese (49) ambaye pia mavazi anayobuni hupendwa na kuvaliwa na mke wa Rais wa Marekani Michelle Obama.
Hii ni moja ya mavazi yaliyobuniwa na Tracy Reese
Kabla ya onesho hilo Flaviana alitweet “I love Tracy Reese,one of Mama Obama fav designers too.Walking for her today and she gave me one of the pieces Mama O has from her last col”.
Picha za Flaviana Matata za onesho hilo zimetokea katika mitandao mbalimbali ya nje ikiwemoHollywood.com.