Young Killer ameendelea kudhihirisha kuwa hakushinda Super Nyota kwa upendeleo, wala hakuotea katika single yake ya kwanza ‘Dear Gambe’ na sasa hajabahatisha katika single yake mpya ‘Mrs Superstar’.
Miongoni mwa mashabiki lukuki wa rapper huyo mdogo kutoka Mwanza ni Rehema Chalamila aka Ray C ambaye ameonekana kuguswa na flow za Young Killer baada ya kuisikia single yake mpya ambayo hakujua ni ya nani.
Rapper Young Killer
Kupitia akaunti yake ya Instagram Ray C aliuliza msanii aliyefanya ‘Mrs Superstar’ ambao yeye ameuita ‘Miss Superstar’, kisha akamwaga sifa zake.
@rayc1982: “ Nani Kaimba huu wimbo wa Miss Superstar!!!Nijulisheni I like his Flow!He is a gud rapper…. “