Dunia yetu kwa sasa imepata mabadiliko makubwa sana, kiasi cha kusababisha tamaduni na desturi zetu kuathiriwa na mabadiliko hayo.
Ingawa ni maeneo mengi yameathirika kutokana na athari za kiutandawazi, lakini kwenye hii mada ningependa kuzungumzia hawa wanawake "wasagaji" au "lesbian".
Binafsi ni miongoni mwa waathirika wa hayo mabadiliko ya kiutandawazi, kwa kuwa binti ambae nimempenda kwa kipindi cha hivi karibuni ndio michezo yake hiyo (usagaji), hivyo katika mahusiano yetu hapo awali, hali ilikuwa ngumu sana maana hata siku moja HAKUPENDA tuongelee mambo ya ngono (ingawa tayari ameni-sign in).
Licha ya hivyo, mara kwa mara amekuwa akizungumzia sana mabinti wenzake wakati wa mazungumzo yetu, ingawa nimekuwa nikijitahidi sana kumtoa kwenye mazungumzo hayo, ila yeye amekuwa akilazimisha tujadili mambo ya aina hiyo, hali iliyonipelekea nikawaulize hao rafiki zake kuhusu hali halisi ya mpenzi wangu. Majibu yalikuwa kama ambavyo nilitarajia (kuwa demu wangu ni lesbian).
Aidha, ikitokea nimetoka nae "out" kula nae raha kwenye maeneo ya starehe, kila aonapo rafiki zake ni lazima awatathmini kwa ukaribu mpaka watu walioko karibu yake wanatambua ni nini anafanya, mara nyingine uenda mbali zaidi mpaka kugusa wenzake maeneo ya makalio kwa kuwachapa kofi.
Sasa ndugu zangu wana MMU katika hali kama hii, jembe nifanye nini?, maana kiukweli ni fedheha kuwa na binti anaetamani wanawake wenzake ingawa nampenda, nifanye nini katika hali kama hii?
Source:Jamii Forums
Kumbuka kutoa maoni yako Hapa Chini....
Tags:
Love and Sex