Microsoft kuinunua Nokia kwa dola billion 7.2


Kampuni ya Microsoft imeingia katika makubaliano ya kuinunua biashara ya simu za mkononi ya kampuni ya Finland Nokia kwa dola za Marekani billion 7.2.
microsoft
Biashara hiyo inatarajiwa kukamilika mwanzoni mwa 2014 na jumla ya wafanyakazi 32,000 wa Nokia watahamishiwa kwenye kampuni ya Microsoft.
“It’s a bold step into the future – a win-win for employees, shareholders and consumers of both companies,” alisema Steve Ballmer, Chief Executive wa Microsoft,
Nokia iliwahi kuwa kampuni iliyoongoza katika biashara ya simu za mikononi lakini mauzo ya yalishuka hadi kufikia 24%.
Wakati Nokia imekuwa ikijikongoja kukabiliana na ushindani kutoka kwa makampuni pinzani ya Samsung na Apple, Microsoft nayo imekuwa ikikosolewa kwa kuwa na speed ndogo katika soko la mobile. Swali ni je mpango huu wa Microsoft kuinunua biashara ya simu za mikononi ya Nokia utaisaidia kuiokoa na kuirudishia heshima sokoni?
Previous Post Next Post