Roberto Mancini amekwenda Uturuki kwa ajili ya kusaini kuifundisha Galatasaray (HM)
KOCHA Roberto Mancini jana amekwenda mjini Istanbul, Uturukikufanya mazungumzo ya kusaini Mkataba wa miaka mitatu kuifundisha Galatasaray utakaokuwa na thamani ya Pauni Milioni 4.6 kwa mwaka.
Mancini, amekuwa 'juu ya mawe' tangu atupiwe virago Manchester City mwishoni mwa msimu na anatarajiwa kutambulishwa kurithi mikoba ya Fatih Terim Jumanne.
Mabingwa hao wa Uturuki pia wamekubali kumlipa Mtaliano huyo bonasi ya Pauni Milioni 5.86 kama watavuka hatua waliyofika mwaka jana Ligi ya Mabingwa na kufanikiwa kuingia Robo Fainali.
Mancini anatarajiwa kukutana na Rais wa klabu, Unal Aysal Jumatatu kufikia makubaliano ya mwisho ya Mkataba, kwa mujibu wa wakala Muzzi Ozcan ambaye alifanikisha kuziunganisha pande hizo mbili, baada ya klabu hiyo kumfukuza Terim.
Credit binzubeiry
Tags:
Sports