MAN UNITED HATARINI KUPOTEZA BONGE LA KIFAA



moyes 6235f
KOCHA David Moyes yuko hatarini kumpoteza kinda Adnan Januzaj mbele ya wapinzani, Manchester City wanaomtaka. (HM)
Kiungo huyo mwenye kipaji amekuwa kwenye utata wa Mkataba na Manchester United karibu miezi sita sasa.
City imekaa mkao wa kula katika kuwania saini ya mchezaji huyo wa Old Trafford, baada ya kuonekana kama wanashindwa kufikia mwafaka.

Januzaj alionyesha ni mkali baada ya kutokea benchi kipindi cha pili katika mechi na Crystal Palace Jumamosi na kuisaidia United kushinda 2-0.
Pia aliingia katika mchezo wa ngao ya Jamii mwishoni mwa mwezi uliopita na kuisaidia timu kushinda.
Lakini mustakabali wake Old Trafford unaweza kuwa mfupi, vinginevyo, kocha Moyes ampe mshahara wa hadhi ya timu ya kwanza ndipo atabaki.
Januzaj, mwenye umri wa miaka 18, anamaliza Mkataba wake mwishoni mwa msimu na hadi sasa amegoma kusaini Mkataba mpya, licha ya majadiliano kuanza tangu Aprili.
Kengele za hatari zimeanza kulia juu ya Mbelgiji huyo, baada ya sasa kuanza kuomba kutolewa kwa mkopo kufuatia klabu ya Blackburn kuonyesha nia ya kumtaka. 
 Credit: Sportmail 
Previous Post Next Post