Sasa Ni miaka 17 imepita toka legend wa Hip hop Tupac Amaru Shakur afariki dunia (September 1996) lakini kazi zake alizozifanya kipindi cha uhai wake zinaendelea kuingiza pesa kutokana na mirahaba ya kazi hizo.
Tupac na mama yake Afeni enzi za uhai wake
Mama yake mzazi na Tupac Shakur amefungua kesi ya kudai kiasi cha dola milioni 1. 1 za mrahaba (royalties) kutoka katika albam iliyotolewa baada ya kifo cha rapa huyo aliyefariki (1996).
Afeni Shakur mwenye miaka 66 amefungua kesi hiyo dhidi ya kampuni ya Entertainment One kwa madai ya kampuni hiyo kuvunja masharti ya mkataba kwa kushindwa kulipa mirahaba ya album ya Tupac “Beginnings: The Lost Tapes,” ambayo ilitoka (2007).
Kampuni ya E1 ilinunua haki za muziki wa Tupac kutoka kwa Death Row Records iliyofilisika (2006) kwa mujibu wa mashtaka hayo.
Afeni ni ‘Co-administrator’ wa kazi za mwanae Makaveli ambaye pia katika mashtaka yake amedai kampuni hiyo irudishe ‘master’ ya kazi zote za Tupac ambazo hazijatoka kwa mujibu wa ripoti ya TMZ.
Album ya ‘The Lost Tapes’ ina jumla ya nyimbo 10 zikiwemo ambazo Tupac alitoa mwaka (1988).