Kuna uwezekano uliwahi kusikia habari kuhusu uwezekano wa mwimbaji Jennifer Lopez a.k.a J.Lo kurudi kuwa jaji wa shindano la kusaka vipaji vya kuimba ‘American Idol’ msimu ujao, lakini sasa imethibitishwa kuwa staa huyo tayari ameshasaini dili hiyo.
Msimu wa 13 wa American Idol hauko mbali kuanza na J.Lo ameshajihakikishia kuongeza dola za marekani million 17.5 katika akaunti yake kwaajili ya kurejea katika meza ya ujaji.
MailOnline imeripoti kuwa kulikuwa na mvutano wa hapa na pale kati ya J.LO na waandaaji kuhusu mshahara wake wa kazi hiyo, lakini hatimaye walifikia muafaka na kukubaliana kiasi hicho, na chanzo kimoja kuongeza kuwa hiyo ni dili kubwa kwa J.Lo inayozidi hata kiwango cha Britney Spears $15 Million anazolipwa kushiriki X Factor.