Good News: Mke wa Black Ryno Ajifungua Mtoto wa Kike



Hatimaye Rapper Black Rhyno amekuwa baba baada ya mke wake kujifungua mtoto wa kike leo Jumanne (September 24).

Black Rhyno akiwa na mke wake wakati wa ujauzito

Black Rhyno ambaye pia ni mdogo wa Professa Jay amesema mke wake amejifungua mtoto wa kike mishale ya saa 7 na nusu mchana wa leo katika hospitali ya Taifa Muhimbili na kuongeza kuwa mama na mwanaye wote wako salama.

Rhyno kupitia facebook yake amepost furaha yake na kumshukuru Mungu kwa zawadi kubwa aliyowajaalia,

“Mwenyezi mungu Amenibariki sana siku ya Leo kanipa zawadi kubwa mnoooooooo! MKE WANGU AMEJIFUNGUA MTOTO WA KIKE saa 7 na nusu hospitali ya Taifa ya Muhimbili mama na mtoto wako fine.ASANTE MUNGU (THANX GOD FOR BLESSING MY WIFE WITH A BaBY GIRL ONE HOUR EARLY”.

Bongo 5 inawapa hongera Black Rhyno na mkewe kwa kupata mtoto.
Previous Post Next Post