BlackBerry yakubali kununuliwa kwa $4.7 billion




BlackBerry jana imesema imekubali kuingia kwenye mkataba na kundi linaloongozwa na kampuni ya Fairfax Financial Holdings kuiuza kwa thamani ya dola bilioni 4.7.



Katika mkataba huo, wawekezaji watapokea dola 9 za cash kwa kila share.

Hata hivyo Blackberry ilisema itaendelea kutafuta namna zingine zinazowezekana wakati mazungumzo na Fairfax yakiendelea.

Ijumaa Blackberry ilitangaza kupunguza wafanyakazi 4,500 duniani kote.

Mkataba huo utamaliza hali ya sintofahamu inayoizunguka kampuni hiyo ambayo Ijumaa iliyopita ilionya kuwa ilipata hasara ya karibu dola bilioni 1.
Previous Post Next Post

Popular Items