GHANA KUKUTANA NA MISRI KUTAFUTA NAFASI BRAZIL


ghana ed4de
Ghana itamenyana na Misri katika mechi za kuamua nchi ya Afrika itakayowakilisha bara zima katika dimba la kombe la dunia mwaka ujao nchini Brazil. (HM)
Misri kama nchi pakee ambayo imeshinda mechi zake zote za makundi za kufuzu kushiriki kombe la dunia, bila shaka imeziweka hofu nchi zengine na bila shaka hakuna ambaye angependa kumenyana nao.
Hii ni kutokana na matokeo ya drawa iliyofanywa na ambavyo nchi za Afrka zitacheza kwenye michuano ya kutafuta mwakilishiu wa bara la Afrika Brazil mwaka ujao.
Mabingwa wa Afrika Nigeria watachuana na Ethiopia wakati Ivory Coast wakitoana jasho na Senegal.
Tunisia, waliofuzu baada ya Cape Verde watachuana na Cameroon.
Burkina Faso, nao waliomaliza wa pili katika michuano ya taifa bingwa Afrika watatoana jasho na Algeria.
Mechi za awamu ya kwanza ya michuano hiyo, zitachezwa kati ya tarehe 11 na 15 Oktoba, huku mechi za marudio zikichezwa kati ya tarehe 15-19 Novemba.
Shirikisho la soka duniani, Fifa, limezitaka nchji hizo kuchangua siku ya mechi, eneo wanalotaka kuchezea na mechi ya kwanza ifikapo Ijumaa wiki hii.
Wakati Ghana wanahisi kutokuwa na bahati nzuri baada ya kuamuliwa kuwa watacheza na Misri, wanaweza kujipa moyo kwani waliwahi kuwashinda Misri kwenye mechi ya kirafiki iliyochezwa Dubai mwezi Januari.
Na haijulikani ikiwa Misri watacheza mechi yao ya marudio mjini Cairo kwani mgogoro wa kisiasa unatokota nchini humo. 

 Credit: bbcswahili 
Previous Post Next Post