Francis Cheka arudi shule ‘Pre-form one’, St Joseph



Yule Bingwa wa dunia wa WBF Francis Cheka ameamua kurejea darasani kujiunga na pre-form one, St Joseph ili kujiendeleza kielimu



Cheka amelimbia gazeti la Mwananchi kuwa hakupata nafasi ya kuendelea na shule kutokana na matatizo ya kifamilia na kuishia darasa la saba, ila kwasasa ameamua kurejea darasani baada ya kupewa udhamini na shule ya St Joseph.

“Nahitaji kuwa Cheka mpya kielimu ili nifike mbali, miaka kumi ijayo hadi namaliza elimu yangu nitakuwa na miaka 41. Hapo nitaamua niendelee na ngumi au nifanye biashara zangu nyingine“. Alisema cheka.

Mpiganaji huyo wa masumbwi pia amefunga kiwanda cha kusaga chupa nyumbani kwao Morogoro baada ya kununua mashine ya milioni 8 hali iliyosaidia kuajiri vijana wasio na kazi zaidi ya ishirini na tano.
Previous Post Next Post