CCM YAWA LULU NYAMONGO TARIME







Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akikata utepe kama ishara ya kufungua ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune,wilaya ya Tarime mkoani Mara.



Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Nyamongo na kuwaeleza namna ambavyo wamejipanga kutatua tatizo la muda mrefu baina ya wakazi wa eneo hilo na wamiliki wa mgodi wa North Mara





Ofisi ya CCM Tawi la Nyabichune wilaya ya Tarime mkoani Mara ambalo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilizindua rasmi leo tarehe 23 Septemba 2013(hd)


Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana alilazimika kupangua ratiba ya ziara ya baada ya kuona kuna jambo la muhimu zaidi angependa kupata muda na wakazi wa Nyamongo ambao wamekuwa na kero za muda mrefu bila kupata majibu.

Baada ya mapokezi katika kijiji cha Mrito, Katibu Mkuu alipokea taarifa ya kamati ya siasa kisha kuelekea katika shughuli ya kufungua Tawi la Nyabichune,mara tu shughuli za ufunguaji Tawi ilipokamilika alipokea taarifa mbali mbali na ndipo akagundua kuna haja ya kupangua ratiba na kwenda kusikiliza ya wananchi.

Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye awaambia mkutano huu ni wa kusikiliza kero na kuzitafutia ufumbuzi kwani CCM peke yake ndio inaweza kutatua hilo tatizo

Naibu Waziri wa Nishati na Madini Ndugu Stephen Masele asitisha huduma ya kulipiwa ada mpaka taratibu na makubaliano yapangwe upya,asikitishwa na watendaji wazembe,azungumzia mpango wa kugawa maeneo kwa wachimbaji wadogo wadogo,awataka waunde vikundi watafute leseni,ahimiza kuna Dirisha la Mikopo TIB Bank,pamoja na serikali kuwasaidia vifaa.

Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana atoa wawakilishi wa wananchi kutoka kwenye mkutano, akaa nao kikao cha ndani pamoja na viongozi wa Serikali ,chama na wananchi

.
Previous Post Next Post