Inaonekana taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa, TAKUKURU inataka kuja na kampeni mpya na huenda ikawatumia wasanii kui’push.

Ben Pol na Ditto wakiwa kwenye ofisi za makao makuu ya TAKUKURU
Taasisi hiyo leo imekutana na wasanii mbalimbali wakiwemo Ben Pol, Lameck Ditto, Nick wa Pili na G-Nako kwaajili ya kikao.

Ben Pol, Nick wa Pili na G-Nako
Bado haijajulikana mkutano huo ulihusu nini lakini kuna uwezekano mkubwa ukawa mkutano wa mwanzo wa kampeni ya taasisi hiyo.