Batulli, Rose Ndauka, Richie na Slim wachaguliwa kuwa mabalozi wa soko la hisa la Dar es Salaam, DSE




Waigizaji wa filamu nchini Yobnesh Yussuph maarufu kama Batulli, Rose Ndauka, Single Mtambalike na Slim Omary wameteuliwa kuwa mabalozi wa soko la hisa la Dar es Salaam, DSE.






Kutoka Kushoto: Rose Ndauka, Slim Omary, Single Mtambalike na Batulli

Batulli Amesema mkataba wa ubalozi wao utadumu kwa kipindi cha miezi tisa.

“Kazi yetu ni kutangaza vipindi vya soko la hisa la Dar es salaam tukiongozwa na Pascal Mayala, matangazo yote tutakuwepo TV, radio na magazeti,” amesema Batulli.


Batulli


“Nimejisikia vizuri sana ni kazi ya heshima kubwa sana kwangu na naamini itanifanya niwe na kipaji kipya cha utangazaji,” aliongeza Batulli.
Previous Post Next Post

Popular Items

HOW TO LOOSE GOOD WOMAN

5 THINGS YOU DON'T KNOW ABOUT LIL COOL J