MSHAMBULIAJI Mario Balotelli ameinusuru AC Milan kulala baada ya kufunga kwa penalti na kufanya sare ya 2-2 na Torino, ambao walikuwa wanapigania ushindi wa kwanza The Rossoneri ndani ya miaka 12. (HM)
Macho ya wengi yalikuwa kwa Kaka, ambaye alikuwa anarejea rasmi Milan baada ya miaka minne ya kuitumikia Real Madrid, lakini Torino ikatangulia kupata mabao mawili kipindi cha pili.
Nahodha, Danilo D'Ambrosio na Alessio Cerci waliifungia mabao hayo Il Toro na kuiatamanisha ushindi wa kwanza dhidi ya Milan tangu Novemba 2001 na Sulley Muntari akaipunguzia Rossoneri bao moja baadaye, kabla ya Balotelli kusawazisha kwa penalti dakika ya 90.
Wakati huo huo, Napoli ilishinda 2-0 dhidi ya Atalanta Uwanja wa Stadio San Paolo na kupanda kileleni.
Tags:
Sports