AGNES MASOGANGE NA MDOGO WAKE AMABAO WANAKESI YA KUKAMAMTWA NA MADAWA YA KULEVYA SOUTH AFRIKA WAACHIWA KWA DHAMANA HUKO AFRIKA KUSINI



Wasichana wawili raia wa Tanzania Agnes Gerald maarufu kama ‘Agnes Masogange’ (25) na mdogo wake Melisa Edward (24) waliokamatwa zaidi ya miezi 2 iliyopita katika uwanja wa ndege wa kimataifa Or Tambo, Afrika Kusini wameachiwa kwa dhamana.
Aggy
Agnes Gerald (Masogange)
Mkuu wa Kitengo cha Dawa za Kulevya Afrika Kusini, Kamishna Toto Mangaleni aliithibitishia MWANANCHI jana kuwa watuhumiwa hao wameachiwa kwa dhamana, lakini wataendelea kubaki Afrika Kusini wakati kesi yao ikiendelea.
Mangaleni alisema wanawake hao ambao juzi pia walipanda kizimbani, walipata dhamana hiyo jana kutoka Mahakama Kuu ya Gauteng iliyoko eneo la Kempton Park jijini Johannesburg.
Hata hivyo, Kamishna Mangaleni alisema hawezi kuzungumzia zaidi kuhusu kesi hiyo kwa sababu hataki kuharibu uchunguzi ambao unaendelea dhidi ya Watanzania hao.
Melisa
Melisa Edward
Marafiki wa karibu wa Masogange wanaoishi maeneo ya Midland Johannesburg ambao walikataa kunukuliwa majina yao, walithibitisha kuwa wanawake hao wameachiwa kwa dhamana.
“Ni kweli wameachiwa leo asubuhi. Lakini hatuwezi kuongelea kwa kina habari hizi kwa sababu hatutaki matatizo na polisi. Hii kesi bado inaendelea na wataendelea kubaki hapa hadi kesi yao itakapomalizika,” alisema mmoja wa marafiki zake.
Habari za kuachiwa kwa Agnes na mwenzake zilianza kusambaa jana baada ya Agnes kuanza kupost picha katika akaunti zake za mitandao ya kijamii.
Kupitia facebook Agnes aliandika:
“Thnanx god nimeamini ww ulikuwa pamoja na mm katika maombi yangu na thnx kwanwote mliokuwa mkiniombea mungu kapokea maombi yenu.”
Agnes fb
Huku upande wa Instagram aliweka picha mpya zilizosindikizwa na captions “I knw kuna watu mm kutoka imewwuma sana ila ninachosema mungu akipanga chake binadamu hawez kupangua sasa polen sana wale wenye roho mbaya “.
Agnes insta
Hizi ndio picha mpya ambazo Agnes Masogange alipost jana kupitia akaunti yake ya Instagram
Agnes-1
Agnes-2
Agnes-3
Naye Mkuu wa Kitengo cha Polisi cha Kuzuia na Kudhibiti Dawa za Kulevya, Godfrey Nzowa aliiambia Mwananchi jijini Dar es Salaam kuwa alikuwa amepata taarifa za kuachiwa kwa wasichana hao, lakini alikuwa anawasiliana na watu wa Afrika Kusini ili kupata uhakika.
Nzowa, hata hivyo alilidokeza gazeti hili juzi kuwa kuna uwezekano wanawake hao wangepata dhamana au kufungwa kifungo chepesi kwani dawa walizokamatwa nazo ni kemikali zinazotumika kutengeneza dawa za aina tofauti kwa matumizi ya binadamu ingawa pia na dawa za kulevya.
Ijumaa ya (July 5), shirika la habari la Afrika Kusini (SABC) liliripoti taarifa juu ya kukamatwa kwa wasichana wawili (ambao baadae walikuja kuthibitishwa kuwa ni Agnes Gerald na Melisa Edward) waliowasili na ndege kutoka Tanzania wakiwa wana mabegi sita makubwa ya dawa zinazoaminika kuwa ni `Crystal Methyl Amphetamine’ maarufu kama ‘Tik’ nchini humo, yenye thamani ya Rand 42.6 million sawa na zaidi ya billion 6 za Tanzania.
Source: MWANANCHI Picha: Instagram:aggnesfineassgirl, Facebook:
Agness Gerlad, Mellis Edward
Previous Post Next Post

Popular Items

EXPENSIVE THING OF THE DAY

New Music: Blue - Pesa