Washika bunduki wa jiji la London, klabu ya Arsenal wamepata ushindi wa kwanza msimu huu baada ya leo hii mshambuliaji wao hatari, Lukas Podolski kufunga mabao mawili kati ya 3-1 waliyoshinda dhidi ya Fulham katika dimba la Craven Cottage.
Kipigo cha mabao 3-1 katika mchezo wa ufunguzi wa ligi kuu soka nchini England dhidi ya Aston Villa katika uwanja wao wa Emirates ulizua maswali mengi kwa mashabiki wa klabu hiyo juu ya kocha wao Arsene Wenger kutokana na kutosajili, lakini ushindi wa leo umezima kelele zote.
Pia ushindi 3-0 wa mechi za hatua ya kwanza ya ligi ya mabingwa barani Ulaya dhidi ya Fenerbahce na ushindi wa leo ambao umechangiwa na bao la kipindi cha kwanza la Olivier Giroud na mabao ya Podolski kipindi cha pili yemepandisha morali kwa wana Arsenal.

Kikosi cha Fulham leo: Stockdale 5, Riether 5, Hughes 5, Hangeland 6, Riise 5, Duff 5 (Bent 59 – 6), Parker 6, Sidwell 6 (Karagounis 75), Taarabt 6 (Kacaniklic 62 – 6), Kasami 6, Berbatov 5
Wachezaji wa akiba: Ruiz, Briggs, Boateng, Etheridge
Bao: Bent 77
Kadi: Parker, Kasami
Kikosi cha Arsenal: Szczesny 6, Jenkinson 7, Sagna 7, Mertesacker 7, Gibbs 7, Ramsey 8, Rosicky 7 (Wilshere 70), Cazorla 7, Podolski 8 (Sanogo 81), Walcott 8, Giroud 7 (Monreal 72)
Wachezaji wa akiba: Fabianski, Frimpong, Gnabry, Zelalem
Mabao: Giroud 14, Podolski 41, 68
Kadi: Ramsey, Wilshere




MATOKEO YA MECHI ZOTE
England: Premier League
Finished | Fulham | 1-3 | Arsenal | (0-2) | ||||||
Finished | Everton | 0-0 | West Bromwich Albion | (0-0) | ||||||
Finished | Stoke | 2-1 | Crystal Palace | (0-1) | ||||||
Finished | Southampton | 1-1 | Sunderland | (0-1) | ||||||
Finished | Newcastle United | 0-0 | West Ham | (0-0) | ||||||
Finished | Hull | 1-0 | Norwich | (1-0) | ||||||
62′ | Aston Villa | 0-1 | Liverpool | (0-1) |
Tags:
Sports