Utafiti: Kupost picha zako mara kwa mara Facebook ni njia ya haraka ya kupoteza marafiki




Kushare picha kwenye Facebook ni njia ya haraka ya kupoteza marafiki, kwa mujibu wa utafiti mpya.
article-2386874-1B34297A000005DC-194_634x411
Watafiti wamebaini kuwa wale wanaopost picha mara kwa mara hujiweka katika uhakika wa kukera wengine. Wanaweza kuharibu uhusiano na marafiki, ndugu na wengine wanaoshindwa kwendana vizuri na wale wanaoshare sana picha zao wenyewe.
Dr David Houghton, wa chuo kikuu cha Birmingham cha Uingereza alisema: ‘Utafiti wetu ulibaini kuwa wale wanaopost picha zao kwenye Facebook mara kwa mara wanahatarisha mahusiano yao ya maisha ya kweli. Ni vizuri kukumbuka kuwa taarifa tunazoziweka kwa rafiki zetu Facebook, huangaliwa na watu wa aina mbalimbali, wapenzi, marafiki, watu wa familia, wafanyakazi/wanafunzi wenzako na kila kundi huwa na mtazamo tofauti kwa taarifa tunazoshare.’
Via: Daily Mail
Previous Post Next Post