Technology: Microsoft kuzindua Windows 8.1 mwezi Oktoba mwaka huu




Microsoft imetangaza kuwa ‘operating system’ ya Windows 8.1 iliyoboreshwa zaidi itaanza kupatikana October 18.


Kwa mujibu wa taarifa kutoka blog ya Microsoft, Kuanzia usiku wa 12:00 am (October 18) Windows 8.1 itaanza kupatikana dunia nzima kama ‘free update’, kwa wateja wenye toleo lililopo la Windows 8 kupitia Windows Store. Windows 8.1 pia itauzwa kwa wateja wapya na itapatikana katika kompyuta zote mpya na tablets kuanzia tarehe hiyo.

Microsoft imetaja vitu vilivyoboreshwa katika toleo la Windows 8.1 kuwa ni pamoja na personalisation, Internet Explorer 11, search powered by Bing, built-in apps, an improved Windows Store experience pamoja na cloud connectivity with SkyDrive. Mabadiliko mengine katika toleo hilo ni Start button imerudishwa katika desktop.

Windows 8.1 inakuja ikiwa ni karibia mwaka mmoja toka Windows 8 iingie sokoni ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Microsoft kuboresha features za windows na bidhaa zake zingine.
Previous Post Next Post