Ray C: ‘Azaliwa mara ya Pili’, asema Shetani hana nafasi tena kwake



Jina la Rehema Chalamila a.k.a Ray C linaendelea kutokea kwenye mitandao kutokana na kile kinachoonekana kuwa mabadiliko katika maisha yake toka aanze kupona kutoka katika matatizo aliyokuwa nayo (madawa), na sasa ameamua kuutafuta utakaso wa kiroho kwa kuzaliwa kwa mara ya pili (kubatizwa).
Juzi (August 29) Ray C ali-share picha kupitia Instagram na tweeter zikimuonesha akiwa anabatizwa , lakini pia alitweet kuhusiana na uamuzi wake huo na kwamba shetani hana tena nafasi kwake.

Hii ndio picha aliyoweka Instagram na twitter ikionesha wakati akibatizwa
Ray C abatizwa
Picha hiyo ilisindikizwa na caption hii “Nimebatizwa Rasmi Leo kanisa la Siloam…Shika neno tenda neno,Shetani huna nafasi tena kwenye Maisha yangu,nimepewa ruksa na Mwenyez Mungu nikukanyage kanyage Usinizoee!!!!Ameeeen!”
Siku za hivi karibuni ‘Uko wapi’ hit maker ameonekana kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yake ikiwa ni pamoja na kuingia gym kwa lengo la kupunguza uzito. Nice Move Rehema Chalamila, kila lakheri katika maisha yako ya kiroho na kimwili.
Previous Post Next Post