Rais wa Kenya Uhuru Kenyatta alikutana na rais wa China Xi Jinping Jumatatu katika ziara rasmi mjini Beijing, inayolenga kuimarisha mahusiano kati ya nchi zao mbili. Wachambuzi wa maswala ya kisiasa hata hivyo wanasema huenda pia rais Kenyatta anatafuta rafiki mwenye ushawishi mkubwa kudhoofisha kesi ya mahakama ya kimataifa – ICC dhidi yake.
Bw. Kenyatta alikaribishwa rasmi na kwa taaadhima kuu na mwenyeji wake rais Jinping akiwa pamoja na wafanya biashara wa Kenya. Ziara hiyo inalenga kujenga mahusiano ya kiuchumi na China na kutafutia bidhaa za Kenya soko nchini humo.
Rais huyo wa Kenya alielezea manufaa ya ushirika wa China na Kenya, akitaja maendeleo na uwekezaji ambao umeimarisha miundombinu nchini mwake hususan barabara.
Bw. Kenyatta alikwenda China baada ya kukutana na maafisa wa Russia mjini Moscow ambapo pia alishuhudia wanariadha wa Kenya wakishindana katika mbio za masafa marefu na kujishindia medali kadhaa za dhahabu.
Bw. Kenyatta alikwenda China baada ya kukutana na maafisa wa Russia mjini Moscow ambapo pia alishuhudia wanariadha wa Kenya wakishindana katika mbio za masafa marefu na kujishindia medali kadhaa za dhahabu.
China na Russia ni wanachama wa kudumu katika baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na ni maarufu kwa kutumia kura ya turufu kupinga miswada yoyote yenye utata wa kisiasa. Maafisa wa Kenya na wale wa Umoja wa Afrika wamekuwa wakiliomba baraza hilo la Umoja wa Mataifa kuiomba mahakama ya kimataifa ICC kurejesha nchini Kenya kesi za uhalifu wa kivita dhidi ya rais Kenyatta na wakenya wengine.
Mchambuzi wa maswala ya kisiasa kutoka chuo kikuu cha Nairobi Adams Oloo aliiambia Sauti ya Amerika kuwa ziara ya rais Kenyatta inatoa ujumbe wazi kuwa Kenya inatafuta washirika wenye nguvu na kwamba haitegemei msaada wake kutoka nchi za Magharibi pekee.
Tags:
Social