Ali Hussain ni mtoto mwenye miaka 14 lakini anaonekana kama mzee wa miaka 110 kwasababu ya tatizo nadra sana duniani linalomfanya akue haraka kuliko kawaida.
Ali ameshuhudia ndugu zake watano wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo uitwao Progeria na ambao unajulikana kwa kuathiri watu 80 tu duniani kote. Kaka zake wawili na dada zake watatu walifariki kwa ugonjwa huo huko kwenye jimbo maskini zaidi nchini India la Bihar.
Ali akipose kwa camera
Progeria humfanya mtu akue haraka na wahanga wa ugonjwa huo wa kurithi huwa na tatizo la arthritis, matatizo ya macha ma moyo. Wale wanaoumwa ugonjwa huo hawatajiwi kuishi zaidi ya miaka 14, lakini licha ya Ali kufikisha umri huo bado hajakata tamaa.
Ali akimsaidia mama yake kuteka maji
“Nataka sana kuishi na nina matumaini kuwa ipo dawa ya tatizo langu. Siogopi kifo lakini wazazi wangu wameteseka sana,” alisema. “Ningependa kuishi miaka mingi zaidi kwaajili yao. Sitaki kuwapa mzigo wa maumivu mengine.”
Wazazi wa Ali, Nabi Hussain Khan, 50, na Razia, 46, ni mtu na binamu yake na walioana kwa kupangiwa miaka 32 iliyopita.
Familia ya akina Ali
Nabia na Razia, wenye watoto nane kwa ujumla wana watoto wawili wa kike wenye afya, Sanjeeda, 20, aliyeolewa na kuzaa watoto wawili. Mtoto wake wa mwisho Chanda, 10, naye hana tatizo hilo.
Ali akilishwa chakula na mama yake, pembeni ni mdogo wake, Chanda
Nabi, anafanya kazi kama mlinzi kwenye kiwanda hulipwa paundi 20 kwa mwezi sawa ni shilingi 50,000. Anasema hawakuwahi kusikia tatizo hilo la Progeria na kwamba madaktari hawakuwahi kusema.
“Kama daktari angetuambia kwamba watoto wetu walikuwa na tatizo la kurithi tungeacha kuzaa,”alisema.
Waliendelea kuzaa kwa matumaini kuwa wangepata mtoto asiye na tatizo na ndipo walipompata Sanjeeda.
Maisha yalikuwa magumu kwa watoto wao wenye tatizo hilo kwakuwa walikuwa wakizomewa shuleni na kuitwa majina kama watoto wenye macho makubwa ama ‘Patlu’ likimaanisha watu wembamba. Hatimaye waliacha kwenda shule. Ali anasema hali hiyo iliwafanya wajifungie tu ndani kwao kuogopa kutaniwa.
Kwa sasa Ali ndio mtoto pekee kwenye familia hiyo aliyebaki na tatizo hilo.
Source: Daily Mail
Tags:
Uncategolized