Picha: Lady Jaydee akutana na Salif Keita wa Mali



Unapozungumzia wanamuziki wakubwa wa bara la Afrika huwezi kuacha kumtaja mwanamuziki mkongwe Salif Keita kutoka Mali.



Lady Jaydee alipata bahati ya kukutana na mkongwe huyo wa Mali jijini Nairobi hivi karibuni, na kupata muda wa kupiga picha pamoja na kufanya mazungumzo ambayo huenda yatakuja kuzaa kitu kitachachowaunganisha wanamuziki hao hivi karibuni.

Jumatatu (August 12) Kupitia akaunti yake ya facebook Lady Jaydee aliandika :
“Nimekutana na SALIF KEITA kwenye breakfast Southern Sun Hotel Nairobi, nimetetemeka nusu niangushe plate yangu..”

Akiashiria tayari kuna mpango wa kushirikiana na mkongwe huyo wa Mali anayefahamika kamaSauti ya dhahabu ya Afrika ‘Golden Voice of Africa’ Jide aliandika “Najaribu tu ku imagine Lady JayDee na Salif Keita kwenye stage moja wooooooooh!! Crazy”.



Jana Jaydee aliendelea kuwajulisha mashabiki wake kuhusu kile kilichotokea na mpango uliopo baada ya kupata nafasi ya kukutana na mwanamuziki huyo mkongwe:
“Leo nimekaa na Salif Keita, Tuka shake hands, tuka hug, tukapiga mapicha mbali na yote kuna kitu kikubwa kinakuja kati yangu na yeke….”.

Salif Keïta aliyezaliwa mwaka (1949) anatambulika kimataifa kama mwanamuziki wa Afro-pop na mtunzi ambaye hufanya muziki uliochanganywa na vionjo vya asili ya Afrika magharibi. Alihamia Paris nchini Ufaransa mwaka (1984) kwaajili ya kuutangaza zaidi muziki wake.

Kutokana na status za Lady Jaydee kuhusu kukutana kwake na Salif Keita kuna dalili za kitu kikubwa kutoka kwao, na hisia zangu zinaniambia yaweza kuwa wimbo wa pamoja au show au vyote.
Previous Post Next Post