Oprah Winfrey aiomba msamaha Switzerland kwa kuihusisha na ubaguzi wa rangi




Baada ya malkia wa talkshow Oprah Winfrey kudai kuwa alioneshwa ubaguzi wa rangi huko Zurich baada ya kushindwa kupewa huduma katika duka la urembo kitu kilichokanushwa na mmiliki wa duka hilo, sasa bunduki imemgeukia Oprah aiomba msamaha Switzerland.



Akizungumza kupitia “The Butler,” Winfrey amesema tukio la Switzerland lilikuwa ni tukio tu na hakutaja jina la duka na kuitaja nchi kitu anachokiri kukosea na kuongeza kuwa alikuwa tu anatolea mfano wa mtu kuwa sehemu ambayo watu wanadhani hauna uwezo wa kuwepo pale.

“I think that incident in Switzerland was just an incident in Switzerland. I’m really sorry that it got blown up, I purposely did not mention the name of the store. I’m sorry that I said it was Switzerland”.

Aliendelea kusema “I was just referencing it as an example of being in a place where people don’t expect that you would be able to be there.”




Upande mwingine mmiliki wa duka hilo la Trois Pommes la Zurich linaloshutumiwa kumbagua Oprah, Trudi Goetz, amedai kutaka kuzungumza na staa huyo haraka iwezekanavyo baada ya Oprah kuiomba msamaha Switzerland, na kusema mfanyakazi wake hakufanya kosa lolote hivyo hatamfukuza kazi.

“I don’t know why she talked of racism. I am sorry, but perhaps she is being a little over-sensitive here. Maybe she was somewhat offended because she was not immediately recognized in the store.” Alisema Goetz

Mkasa huu ulianza baada ya Oprah kupitia Entertainment Tonight kudai kubaguliwa na muuzaji wa duka la urembo huko Zurich mwezi mmoja uliopita, kwa kukataa kumuonesha mkoba uliokuwa unauzwa $38,000 kwa kumwambia ni wagharama kubwa ambayo hataiweza, bila kujua alikuwa akiongea na bilionea na staa wa talk show.
Previous Post Next Post