NMB yatwaa Tuzo ya Benki Bora Tanzania






Dar es Salaam. Benki ya NMB imetajwa kuwa Benki Bora Tanzania kwa mwaka 2013.
Tuzo hiyo ilitolewa na Jarida la Euromoney linalojihusisha na masuala ya fedha, kwenye hafla mjini London, Uingereza.
Mwaka 2012, NMB ilitajwa  kama taasisi iliyofanya vizuri kwa kutoa huduma za fedha, kuweka mitaji na zaidi kusaidia wateja kwenye masuala ya benki na ujasiriamali.
Akizungumzia tuzo hiyo, Mhariri wa Jarida la Euromoney, Clive Horwood, aliisifu benki hiyo kuwa kati ya zinazopiga hatua Tanzania na kwamba, hiyo imesukumwa na kutawala asilimia 40 ya wateja wa benki mbalimbali nchini.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa NMB, Mark Wiessing,  alionyesha kufurahishwa na tuzo hiyo kutoka Euromoney na kwamba,  hizo ni jitihada za utendaji mzuri wa wafanyakazi na menejimenti.
NMB yenye matawi 150 Tanzania na wateja milioni 1.8, kwa sasa imesambaa  wilaya mbalimbali kwa asilimia 95, huku asilimia 60 ya matawi yake yakiwa maeneo ya vijijini.

Chanzo via: Mwananchi
Previous Post Next Post