Mashindano ya Miss Utalii yapigwa ‘Stop’



MTANZANIA limeripoti kuwa bodi ya Taifa ya Miss Tourism Tanzania Organisation (MTTO), imetangaza kusimamisha kufanyika mashindano hayo katika ngazi zote kwa msimu wa 2013/2014 kwa lengo la kujipanga upya na kuboresha mfumo wa uendeshaji na usimamizi wa mashindano hayo.



Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari na Mwenyekiti mtendaji wa kampuni hiyo, Erasto Chipungahelo, amesema uamuzi huo mgumu umechukuliwa katika kikao cha bodi hiyo kilichofanya tathimini ya miaka mitano ya Miss Utalii Tanzania.

Mashindano ya Miss Utalii Tanzania yalifanyika kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee na fainali za tano zilifanyika Mei 2013, jijini Tanga kwenye Uwanja wa Mkwakwani.

Bodi katika tathimini hiyo imebaini changamoto mbalimbali za kimfumo, utendaji na hujuma na pia imebaini sanaa ya urembo kudumaa au kutokua kwa kasi inayotakiwa ukilinganisha na nchi jirani na hata nyinginezo duniani.

SOURCE: MTANZANIA,
Previous Post Next Post