Wachezaji wa Man united wakiwa na ngao ya jamii mara baada ya kuitungua Wigan 2-0 (HM)
Robin Van Persie
MABAO mawili ya Mdachi, Robin Van Persie yameiwezesha Manchester United kuilaza 2-0 Wigan kwenye Uwanja wa Wembley na kutwaa Ngao ya Jamii.
Ushindi huo ni faraja na mwanzo mzuri kwa kocha mpya wa United, David Moyes aliyerithi mikoba ya Sir Alex Ferguson aliyestaafu mwishoni mwa msimu uliopita.
Van Persie alifunga bao la kwanza dakika ya saba kwa kichwa cha nguvu, akiunganisha krosi ya Patrice Evra kutoka wingi ya kushoto na akafunga la pili dakika ya 59 baada ya kufumua shuiti lililombabatiza beki wa Wigan, James Perch.
Kikosi cha Man Utd kilikuwa: De Gea, Rafael/Smalling dk16, Jones, Vidic, Evra, Zaha/Valencia dk61, Carrick, Cleverley, Giggs/Anderson dk67, Welbeck/Kagawa dk83 na Van Persie/Januzaj dk84.
Wigan: Carson, Boyce, Perch, Barnett, Crainey, McCarthy/Dicko dk86, Watson/Espinoza dk71, McArthur/McCann dk61, Maloney/Gomez dk71, Holt/Fortune dk61 na McClean/McManaman dk62.
Tags:
Sports