Kutoka Zanzibar; Shilingi milioni 100 kutolewa kwa atakayesaidia kukamatwa watuhumiwa wa matukio ya tindikali



Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, limetangaza dau la Shilingi milioni 100 kwa mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa za kundi la uhalifu linalojihusisha na vitendo vya kuwamwagia maji baadhi ya watu yanayodhaniwa ni tindikali
_MG_4099
Kamanda wa Polisi Kanda hiyo, Suleiman Kova, alisema vitendo hivyo havipaswi kuvumiliwa na kuwaomba wananchi kutoa ushirikiano kwa kuwafichua watu hao.
“Nimeamua kuomba fedha hizi serikalini ili nimpe mtu atakayewezesha kupatikana kwa taarifa hizo, hatimaye kukomesha vitendo hivi. Kemikali hii imekuwa na madhara makubwa,” alisema Kova.
Hivi karibuni Mkurungezi wa Maduka ya Home Shopping Center wa Dar es salaam na Mfanyabiashara wa Lebonon na raia wawili wa Uingereza walimwagiwa maji yanayodhaniwa ni tindikali huko Zanzibar.
Source: Mwananchi
Previous Post Next Post